Hayo ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Waziri Kindamba aliyoyatoa kwa wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri leo Februali 07, 2023 alipokuwa akifungua kikao cha tathimini ya utendaji wa halmashauri za wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa.
Mhe.Kindamba ameongeza kuwa kufanyika kwa mikutano ya kisheria katika vijiji kunapunguza kero na malalamiko mengi ya wananchi ambayo yanaweza kumalizwa na viongozi wa ngazi za chini lakini yamekuwa yakisubiri majibu kutoka ngazi za juu hali inayoharibu dhana ya utawala bora.
Ameongeza kuwa licha ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuendelea na kutoa mamilioni ya pesa za miradi bado wananchi wanahitaji kutatuliwa changamoto walizonazo kupitia mikutano ya hadhara ambayo ni haki yao ya kisheria.
Kupitia mikutano hiyo wananchi hupata taarifa mbalimbali zikiwemo za pesa za miradi zinazotolewa na Mama Samia katika sekta mbalimbali za maendeleo.
“Nendeni kwenye halmashauri zenu kila mmoja kwa nafasi yake kufuatilia iwapo mikutano ya kisheria inafanyika hoja na kero zinazoiibuka zinatolewa majibu na zile zinazowazidi zinapelekwa ngazi husika badala ya kuacha zikiwasumbua wananchi mioyoni mwao zikisubiri ziara za viongozi wa juu”Alisisitiza Mhe,Kindamba.
Mkoa wa Songwe ulio mchanga kuliko yote hapa nchini tangu kuanzishwa kwake una wilaya nne na halmashauri za wilaya tano na tumekuwa tukishuhudia viongozi wa mkoa huo wakihaha kuhakikisha kuwa umri wa kuzaliwa si kikwazo cha maendeleo.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa