Makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo Jumatatu 17/05/2021 katika Gereza la Wilaya hiyo mjini Itumba yakishirikisha viongozi wa Jumuiya ya Wanawake mkoa na Wilaya pia Kamati ya Usalama Wilaya.
Justina Hasunga Mwenyekiti wa UWT mkoani humo amesema kuwa baada Mhe.Mwandawila kutembelea gereza hilo siku chache zilizopita aliguswa na kero ya upungufu wa vifaa hivyo akiahidi kulifanyia kazi ambapo leo ametimiza ahadi hiyo.
Matias Mizengo Katibu Tawala waWilaya hiyo ameshukuru kwa msaada huo akiahidi kuwafikishia walengwa sawasawa na maombi yalivyokuwa yametolewa.
Mkuu wa Gereza hilo Kamishana Msaidizi wa Magereza ACP Joseph Mkude ameshukuru kwa msaada huo akitoa wito kwa wadau wengine kuunga juhudi hizo .
Kiongozi huyo pia aliwaeleza wajumbe hao juu ya ujenzi wa uzio wa gereza unaondelea kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya serikali katika ujenzi wa Taifa kwa kutumia
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa