Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe (Mh. Joseph Modest Mkude) amewahamasisha viongozi na wananchi wote wilayani kujitokeza kuulaki, kuushangilia na kukimbiza Mwenge wa Uhuru pindi utakapo ingia wilayani Ileje. Akiongea katika kikao cha maandalizi ya mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 wilayani hapa kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara, Vitengo na Viongozi wa Taasisi mbali mbali amesisitiza kwa viongozi wote kuwahamasisha wananchi wote wilaya hapa kujitokeza kwa wingi maeneo yote ambazo Mwenge wa Uhuru utapita kwa ajili ya kuushangilia na kuukimbiza.
Pia alisisitiza kuwa maandalizi yote yakamilike kwa wakati na kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwa wingi katika kijiji cha Itumba ambapo mkesha wa Mwenge wa Uhuru utafanyika hapo. Mwenge wa Uhuru unatarajia kuingia Wilayani Ileje tarehe 13/04/2017 utapokelewa kata ya Mbebe na kupita kata ya Chitete, Isongole, Itumba, Ndola, Itale na Mkesha utafanyika kata ya Itumba na siku ya tarehe 14/04/2017, Mwenge wa Uhuru utaondoka Wilayani Ileje na kuelekea wilayani Mbozi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa