DC-Ileje apiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni,wachungaji na machifu waunga mkono waomba sheria ya kufungua vilabu vya pombe izingatiwe waongeza wanaovaa “kata K” pia washughulikiwe.
Mteule huyo wa Rais Ndg Joseph Mkude alitoa agizo hilo wakati wa kikao na Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA) kilichofanyika katika Kijiji cha Isoko Kata ya Kafule kikijumuisha viongozi wa dini machifu na wazee maarufu toka Tarafa ya Bundali ukiwa ni mwendelezo wa vikao hivyo vinavyolenga kuifanya wilaya ya Ileje kuwa makazi salama kwa wote.
“Kuanzia sasa ni marufuku kwa watoto kuonekana vilabuni,naagiza kwa watendaji wa kata,vijiji,wazazi na wananchi kwa ujumla,hata kwa watoto wanaobebwa kwani mazingira hayo si rafiki”alisisitiza kiongozi huyo.
Alisema kuwa ubongo wa mtoto anayeshinda maeneo ya vilabuni hauwezi kuepukana na tabia za ulevi kwa vile anaona na kushuhudia namna maisha ya kiulevi yanavyoendeshwa hali atakayoendeleza hata shuleni na hivyo kuzalisha raia wasio wema na kuwa mizigo kwa jamii.
Awali,Paroko Laymond Kapala wa Parokia ya Ipoka aliomba wazazi na walezi wasiwaogope watoto kwasababu ya viwango vyao vya elimu ikiwemo ya Chuo Kikuu.
“Ndugu zangu mmomonyoko wa maadili haujawaacha hata wasomi,sote tunaona vijana wetu wa Vyuo Vikuu wanavyoenenda hata kimavazi hakuna tofauti kati ya msomi na asiye msomi.
Alisema kuwa kamwe mtoto hakui kwa mzaziye hivyo ni jukumu la kila mwanajamii kuvaa viatu vya ulezi ili kuepukana na kupoteza maadili yetu mazuri ya Mtanzania.
Naye Mchungaji Peter Mwakamele wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Isoko aliomba serikali itoe tamko juu ya mavazi ya aibu yanayovaliwa na vijana wakiwemo watumishi wa serikali ukiwemo mtindo wa “kata K”ambao huonesha nguo za ndani kwa wanaume.
Kikao hicho kililenga kujadili kasi ya imani ya” rambaramba” ambalo limeanza kutishia hali ya usalama ya wilaya pamoja na hifadhi ya mazingira kwa serilkali na kwa kuwatumia machifu ambao zamani waliweza kufanikiwa sana.
Huo ni mwendelezo wa vikao katika kutoa elimu kwa jamii na kupata maoni namna maovu yanavyoweza kukomeshwa katika jamii ambapo Mkuu wa Wilaya alishafanya mkutano kama huu kwa Tarafa ya Bulambya ambapo viongozi wa MUJATA Wilaya ya Ileje walimweleza jinsi wanavyoshirikiana na machifu wa nchi jirani ya Malawi katika kupiga vita maovu yakiwemo mauaji ya imani za kishirikina na albino.

Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa