Gidarya amewataka vijana hao kutumia stadi walizozipata katika kuonesha uzalendo wao kwa taifa kivitendo wakilinda mipaka ya nchi usalama wa raia na mali zao badala ya kutumia mafunzo hayo kunyanyasa wananchi.
“Ni Imani yangu kuwa mafunzo haya yamewajengea ukakamavu,ujasiri na kujiamini mkiwa tofauti na walioshindwa kuvumilia hadi mwisho wakakimbia”Alisema kiongozi huyo.
Meja Winfred Msheri,Mshauri wa Jeshi hilo wilayani humo alisema kuwa jumla ya vijana 135 walianza mafunzo hayo huku wakihitimu 104 wakiwemo wa kike 8 tu akieleza sababu za utoro pamoja na utovu wa nidhamu kuwa chanzo.
Aidha,Meja Msheri alimweleza Mgeni Rasmi kuwa kuwepo kwa idadi hiyo ndogo ya wahitimu kunatokana na imani potofu iliyojengeka kwa baadhi ya wananchi kuwa mafunzo hayo ni mateso hali iliyosababisha baadhi yao kukimbilia wilaya za jirani kwa lengo la kujificha.
Wahitimu hao,kupitia risala yao iliyosomwa na Shangwe Msokwa wameishukuru serikali kwa kuwajengea uzalendo,ukakamavu pamoja na stadi mbalimbali za maisha wakiahidi kuyatumia kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kila mwaka mafunzo kama hayo hufanyika kwa kata moja kwa wilaya nzima ambapo kwa miaka ya hivi karibuni tayari yalishafanyika katika kata za Ngulugulu,Chitete,Mbebe,Itumba,Ngulilo pamoja na Ibaba
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa