Hatimaye serikali imeondoa kero kubwa ya siku mbili iliyokuwa imekata mawasiliano kati ya Isongole na Itumba Makao Makuu ya Wilaya ya Ileje baada ya daraja linalounganisha vijiji hivyo viwili kuvunjika,huku wanchi wakipongeza kasi ya utatuzi huo.
Serikali kupitia TANROAD mkoa wa Songwe wakiwa bega kwa bega na Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg.Joseph Mkude walikuwa wakihaha huku na kule kuhakikisha mawasiliano hayo yakirudi haraka.
Mwandishi wa habari hizi aliyekuwa akifuatilia kila kinachoendelea kwenye eneo la tukio alishuhudia mafundi wakifanya kazi hadi giza kuwaondoa hali iliyopongezwa na wanachi wengi .
Akizungumza name akiwa anaelekea Isongole kwenye mnada Philimon Ngambo mfanyabiashara wa Itumba alisema kuwa hawakutegemea kama utatuzi huo ungefanywa kwa siku mbili kwani huko nyuma hali hiyo ingechukua hata mwezi mmoja.
Lovemore Mwatwambo dreva bajaj,mmoja wa watumiaji wa daraja hilo kila siku alisema kuwa kwa muda mfupi hali hiyo iliwathiri wengi hasa wale abiria waliokuwa hawajui tatizo hilo ambao walijikuta wakilipa nauli karibu mara mbili ya iliyokuwa imeoeleka.
Hata hivyo kijana huyo alitoa ushauri kwa mamlaka husika kuwa na utaratibu wa maram kwa mara wa kukagua madaraja katika msimu huu wa badala ya kusubiri madhara yatokee.
Awali baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo walieleza jinsi walivyoweza kuathirika na tatizo la daraja hilo hasa katika kipindi hiki ambacho kuna maandalizi ya Krismas na Mwaka Mpya.
Daraja hili lipo kwenye kijito Nakambekeswa karibu na Sekondari ya Serikali ya Ileje na linaunganisha pia kwenye barabara za Wilaya za Mbeya Vijijini ,Mbozi na nchi jirani ya Malawi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa