Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika Shule ya Sekondari Loleza Jijijini Mbeya yakiwa ni sehemu ya maandalizi au mwanzo wa mradi huo mkubwa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (World Bank) kwa kutengewa zaidi Trilioni na jumla ya madarasa elfu 12 yakitarajiwa kujengwa.
Akizungumza na washiriki hao Mratibu wa Mradi huo Ngazi ya Taifa Ndg.Yusuph Omary alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watalaam hao ambao ni waundaji wa timu za halmashauri katika kutekeleza mradi huo wa miaka mitano ukitarajiwa kukamilika mnamo 2026.
Katika mafunzo mada mbalimbali zimeweza kutolewa zikiwemo za mapato na matumizi ya fedha za mradi,maana ya mradi,lengo kuu la mradi,uboreshaji wa umahili wa walimu,kuimarisha TEHAMA katika vituo vya walimu na katika shule teule na umuhimu wa kushirikisha jamii katika utekelezaji wa mradi huu mkubwa.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwapa elimu hiyo kabla hawajaanza kutekeleza mradi huo.
Washiriki hao ni kutoka Elimu Msingi,Idara ya Fedha,Kitengo cha Manunuzi,Maendeleo ya Jamii,Ujenzi,Mipango Tume ya Utumishi ya Walimu (TCS)Wathibiti Ubora wa Elimu pamoja na Maafisa Habari.
Mafunzo ya aina hiyo yametolewa na serikali kwa uratibu wa O-TAMISEMI kwa kanda zote tisa hapa nchini huku ukitarajiwa utekelezaji wake kuwa wa kiushindani katika ngazi mbalimbali yaani mikoa,halmashauri hadi kwenye ngazi ya shule utakakokuwa mradi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa