Vitambulisho 3500 kugawiwa kwa wajasiliamali Wilayani Ileje,huku TRA wakiwataka Watendaji wa Kata kuzingatia maagizo ya serikali ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.
Akizungumza kwenye kikao cha siku moja kilichojumuisha watalaam toka Ofisi ya DED pamoja na Watendaji wa Kata Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg.Joseph Mkude alisema kuwa vitambulisho hivyo ni pungufu ya vitambulisho 5600 vilivyouzwa mwaka jana kutokana na kuwa na takwimu za wajasiliamali tofauti na ilivyokuwa mwaka uliopita.
Kiongozi huyo aliwataka wasimamizi wa zoezi hilo kuhakikisha wanalisimamia kulingana na maelekezo ya serikali pasipo kuwanyanyasa wananchi .
Ndg.Haji Mnasi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo aliahidi kusimamia vema zoezi hilo ili kuleta matokeo chanya kwa serikali.
Alisema kuwa wale wenye sifa walio na mauzo yasiyozidi milioni nne kwa mwaka watapata vitambulisho hivyo na kuwandeleza ili kufufikia hatua zingine kibiashara.
Wilaya ya Ileje ina kata 18 hivyo watendaji wa kata hizo waliweza kugawiwa vitambulisho kulingana na takwimu za wajasilamali kwa eneo husika.
Utaratibu wa kugawa vitambulisho vya aina hiyo hapa nchini uliamza mwaka jana lengo la serikali likiwa ni kuwalinda wafanyabishara wadogo na kuongeza mapato ya kiserikali.
Zoezi hili ambalo linafanyika kidijitali linasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya huku utekekezaji wake ukifanywa na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa