Katika kufanikisha zoezi hilo vikao vya kuwekeana mikakati ili kufikia malengo vimeanza leo Jumanne28/12/2021 katika Ukumbi wa Hotel ya VIM iliyopo Itumba Makao Makuu ya Wilaya hiyo vikitarajiwa kuendelea hapo kesho Jumatano 29/12/2021.
Akifungua kikao cha leo kilichohusisha Ofisi ya Elimu Msingi Wilaya pamoja na Maafisa Elimu Kata Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Geofrey Nnauye amewataka watalaam hao kutumia taaluma hiyo kuhakikisha wanawatendea haki wanaileje kwa kuleta mabadiliko makubwa katika matokeo mbalimbali ya mitihani.
Ameongeza kuwa kufanya kazi kwa kusubiri kusimamiwa badala ya kufuata miongozo ya taaluma na serikali,kunachangia matokeo mabaya ya elimu msingi mwaka hadi mwaka hali inayosababisha wilaya hiyo kusomeka vibaya kwa watanzania.
Nnauye amesema kuwa mshikamano,ubunifu na kujituma havina budi kuchukua nafasi ili kuleta matokeo mazuri ambayo yataleta heshima pia kwa wanataaluma hao.
Naye Afisa Elimu Msingi Mwalimu Fikiri Mguye amesema kuwa amedhamiria kwa dhati kuhakikisha kuwa wilaya hiyo inakuwa miongoni mwa wilaya zinazofanya vizuri kitaaluma akitumia mbinu shirikishi katika kupanga na kutekeleza mikakati hiyo.
Amesema kuwa wadau mbalimbali kutoka ngazi za chini hadi juu kiwilaya hawana budi kushirikishwa kupanga na kutekeleza mipango ya uboreshaji elimu ambayo kwa kufanya hivyo ni utekelezaji wa Utawala Bora hapa nchini.
Kwa upande wao Maafisa Elimu Kata hao wameushukuru uongozi wa Wilaya kwa mambo mazuri ya kuwathaminiwa yaliyooneshwa na uongozi wa wilaya kwa muda mfupi.
Phares Kibona Mwenyekiti wa Maafisa hao alishukuru Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Anna Gidarya,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Idara ya Elimu Msingi na Sekondari kwa ushiriki wao wakati wa msiba wa mtoto wa mwalimu aliyekuwa amepoteza uhai kwa kugongwa na gari akiwa amepakiwa kwenye pikipiki na baba yake mzazi ambaye ni mwalimu na alipata majeraha.
Pongezi za pili zilikuwa ni namna walivyokuwa wamethaminiwa katika kikao hicho kwa kukifanyia katika ukumbi wenye hadhi tofauti na vikao vilivyowahi kupita.
Kikao hicho kilichoanza jioni kutokana na sababu zisizozuilika kilikuwa kikiendelea tulipokuwa tukiingia mitamboni na hapo kesho kikao kama hicho kitafanyika kikihusisha Maafisa hao pamoja na Walimu Wakuu.
Kwa miaka kadha Wilaya ya Ileje imeendelea kufanya vibaya kwenye mitihani mbalimbali ya kitaifa hali iliyoendelea kupigiwa kelele na wadau mbalimbali wakiwemo wasomi waliosoma Ileje miaka ya nyuma wilaya hiyo ilipokuwa ikifanya vema.
Hayo yakijili,Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.Omary Mgumba hapo jana aliwataka viongozi wa mkoa huo na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kuwa watoto wote walioandikishwa kuanza Darasa la Kwanza hapo mwakani wanafanya hivyo pia kwa wale waliochaguliwa kuanza Kidato Cha Kwanza.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa