Uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Isongole hadi Isoko umefanyika leo Juni 13, 2025, katika kijiji cha Chabu, kata ya Bupigu wilayani Ileje. Mradi huu mkubwa unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 74.167 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 27 na nusu.
Kukamilika kwa barabara hiyo kutaiwezesha wilaya ya Ileje kufunguka kiuchumi na kijamii, huku likiwa ni chachu ya kuimarisha shughuli za usafirishaji na kuongeza pato la wananchi. Hafla ya uzinduzi ilitanguliwa na dua maalum, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Afisa Tarafa wa Bulambya Bi Irene Lymo, Afisa Tawala wa Wilaya ya Ileje Donbosco Komba, pamoja na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Songwe.
Shukurani na pongezi nyingi zimuendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa barabara hii. Kwa hakika, fikra bunifu… Ileje inafunguka!
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa