Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe 7, Agasti, 2020 na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo Ndg.Haji Mnasi alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wapatao 36 kutoka kata zote za Jimbo hilo la Ileje.
Mnasi amesema kuwa dhamana waliyopewa baada ya kuchujwa vizuri pamoja na viapo ni imani ya Tume kuwa watavitendea haki vyama vyote vya siasa.
Msimamizi huyo ameongeza kuwa,kuingiza itikadi za kisiasa kwa watendaji hao wa tume kunaweza kuzua malalamiko mengi hivyo kuathiri uchaguzi pamoja naTume ya uchaguzi kutoaminiwa
Aidha,amewataka wasimamizi hao kuvishirikisha vyama vya siasa na wadau wa siasa katika mambo wanayotakiwa kushirikishwa kwa mujibu wa miongozo ya tume pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naye Afisa Uchaguzi wa Jimbo hilo Ndugu Pastory Mashiku amewatahadharisha wasimamizi hao kujiepusha na utoaji wa taarifa hasa kipindi hiki cha kidijitali kupitia mitandao ya kijamii hali aliyosema inaweza kuwatia hatiani kwa mujibu wa viapo vyao.
Hivi karibuni taifa la Watanania watapata fursa ya kuchagua Rais,wabunge na madiwani ukiwa ni Uchaguzi Mkuu wa sita tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mnamo mwaka 1992 wakati wa Awamu ya pili ya Mzee Ali Hasan Mwinyi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa