Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Anna Gidarya ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kutokana na wenyeji wake cha siku moja kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Radiwelo aliwataka wajumbe kujadili kwa kina agenda za kikao hicho kwa manufaa ya pande hizo mbili.
Pia Gidarya alitoa wito kwa wajumbe kushiriki kwa vitendo baadhi ya mambo yanayoimarisha mahusiano kama vile michezo kwenda sanjali na kikao kijacho ambacho kinatarajiwa kufanyika katika wilaya ya Chitipa kwenye nchi hiyo iliyo pia mwananchama wa SADC, AU,Jumuia ya Madola pamoja na UNO kama ilivyo kwa Tanzania.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chitipa Mhe.MacMillan Magomero alisisitiza juu ya kufanyika kwa vikao vya aina hiyo vitakavyoleta tija kwa maisha ya wakazi wa wilaya hizo jirani na kwa mataifa hayo mawili ya Tanzania na Malawi.
Hata hivyo kiongozi huyo toka Malawi aliwatahadharisha wajumbe kuzingatia kuwa si kila kitu kinaweza kujadiliwa katia vikao hivyo kwa vile mambo mengine ni ya ngazi za juu za uongozi.
Katika kikao hicho watalaam waligawanyika katika makundi ya kiidara na kisekta ili kuweza kubadilishana uzoefu kisha kutoa mrejesho kwa kikao ili kujenga uelewa wa pamoja.
Mahusiano ya Tanzania na Malawi kupitia mpaka wa Malawi ni ya muda mrefu huku baadhi ya miradi ya maendeleo ikionesha kuimarisha mahusiano hayo.
Miradi hiyo ni pamoja na barabara ya Mpemba hadi Isongole iliyojengwa kwa kiwango cha lami inayoendelea kuongeza watumiaji wa pande hizo mbili siku hadi siku,huku mradi wa Bonde la Mto Songwe ukiendeshwa kiushirika nan chi hizi mbili.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa