Dodoma-Tanzania
Watalaam saba kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wapo kwenye Umbi wa UDOM Jijini Dodoma wakiungana na Halmashauri zingine za mpaka wa Magharibi wa Tanzania pamoja na Mkoa wa Dodoma wakipata mafunzo ya Afya ya Pamoja(One Health Team) kwaajili ya kukabiriana na virusi vya corona na ebola.
Akifungua mafunzo hayo ya siku nne Mkurugenzi wa Idara ya Manejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Matamwe ameitaka jamii kuzingatia mafunzo na maelekezo yanayotolewa na mamlaka husika katika kulikabiri janga la corona linaloitikisa Dunia kwa sasa.
Alisema kuwa yapo maelekezo ya kitaalam yanayotolewa kupitia njia mbalimbali za mawasiliano lakini baadhi ya watu wanayapuuzia hali inayoweza kuchangia kuenea kwa magonjwa hayo.
Katika mafunzo hayo Wilaya ya Ileje inawakilishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya,Afisa Mazingira,Bwana Mifugo wa Wilaya Afisa Habari wa Wilaya,Afisa Misitu,Mtalaam wa Maabara na Mtalaam Maalum Kutoka Idara ya Afya(IDSR Focal Person)
Huko hayo yakiendelea kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma tayari Serikali ya Tanzania kupitia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa imetangaza kuzifunga shule zote kuanzia ngazi ya Chekechea hadi Kidato cha Sita.
Mpaka sasa kwa mujibu wa mamalaka husika ni mtu mmoja aliyeweza kubainika kuwa na virusi vya corona hapa nchini tangu kuzuka kwa janga hili huko nchini China siku kadha ziliopita.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa