Mkuu wa Wilaya ya Ileje ahamishia kwa muda ofisi yake kijijini lengo likiwa kuokoa wanafunzi watakaoanza Kidato cha Kwanza hapo mwakani.
Zoezi hilo lililochukua takribani masaa manne lilifanyika katika Sekondari ya Kata ya Mbebe likiwezeshaKupatikana jumla ya mifuko 79 ya saruji huku kila mmoja akichangia mfuko mmoja ikiwa ni kuanzisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vinavyopungua.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Haji Mnasi aliongoza mjadala kwa Wakuu wa Idara na Vitengo na kukubaliana kila mmoja kuchangia mfuko mmoja wa saruji ambapo jumla ya mifuko 35 iliweza kupatikana.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya na timu yake waliweza kufika sehemu ya tukio wakiwa na mifuko 12 ambayo ilichangiwa na kila mjumbe.
Zoezi hilo lnalenga kuokoa wanafunzi watakaoanza Kidato cha Kwanza hapo mwakani huku shule hiyo ikikabiriwa na upungufu wa vyumba viwili vya madarasa.
Akizungumza baada ya zoezi hilo Diwani wa Kata hiyo Mhe.Andrea Kalinga alieleza kuwa pia Kamati ya Maendeleo ya Kata hiyo “WADC” imechangia mifuko 12 huku kukiwa na mifuko 20 iliyokuwa imebaki kwenye ujenzi wa awali.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa