Akizungumza na timu ya wanafunzi,makocha pamoja na maafisa Elimu Msingi katika kituo hicho Mhe.Mgomi amesisitiza juu ya wasimamizi wa wanafunzi hao kuhakikisha wanalinda usalama wao ili kuwaepusha dhidi ya vitendo vya unyanyasaji vinavyoweza kutokea katika mkusanyiko huo.
Amewasisitiza wanafunzi hao wa shule za msingi ambao wate ni watoto wanaohitaji uangalizi wa karibu kuwa wasiwe wanakaa kimya pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na mtu yeyote wakati wa mashindano hayo na hata watakaporudi makwao bila kujali mahusiano yao hata kama ni mzazi.
Amewataka pia wanafunzi hao kuwapokea wenzao kutoka halmashauri zote tano za Mkoa wa Songwe ili michezo hiyo iwe sehemu ya kuitangaza vema wilayani,huku akiwataka kuiletea ushindi wilaya badala ya kuwa waandaaji tu na washiriki.
Hapo kesho Jumanne 16, Mei, 2023 wamamichezo wa shule za msingi kutoka halmashauri zote za mkoa huu watawasili tayari kwa michezo inayotarajiwa kuanza hapo Mei, 17,2023
Michezo mbalimbali inatarijwa kushindaniwa likiwemo soka kwa wavulana na wasichana riadha,mpira wa pete,kikapu,wavu kwaya muziki wa kizazi kipya na michezo mingine.
Akizungumza wakati wa kumribisha kiongozi huyo Afisa Elimu Msingi Mwl.Fikiri Mguye amesema kuwa timu zote zimeandaliwa vema na walimu (makocha) 12 ambao walishiriki kuchagua wachezaji na kuandaa timu hizo.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa