Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Chabu Kata ya Bupigu wilayani hapa kwa kujitolea katika ujenzi wa miradi katika Zahanati yao kwa nguvu ya wananchi yenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu ikiwa ni thamani ya tripu 10 za mchanga pamoja na uchimbaji wa mashimo manne (4).
Zahanati ya Chabu ilipokea kiasi cha 69,391,897.43/= mnamo tarehe 15/11/2023 kwa lengo la maboresho ya ujenzi wa miundombinu ya usafi na mazingira. Ujenzi wa miundombinu kusudiwa inajumuisha vyoo matundu 6 (2 wagonjwa, 2 wahudumu, 1 wajawazito na bafu moja, 1 wagonjwa wenye mahitaji maalumu), Kichomea taka, Shimo la majivu, Shimo la kondo la mama na uzio wake, Kitakasa mikono, Uwekaji wa mfumo wa maji
Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo Dkt. Diannaeose Massawe, hadi sasa mradi huo umetumia jumla ya Tsh 50,672,900 sawa na asilimia 73.2 na fedha iliyosalia kiasi cha 18,718,997.43 kitaendelea kutumika kwa shughuli zilizosalia. Aidha mradi umefikia wastani wa asilimia 93.125
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa