Katika ukaguzi huo wilayani Ileje imefurahishwa na baadhi ya miradi na kukerwa na miradi mingine kutokana na inavyojengwa.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti chama hicho mkoa Komredi Radiwelo Mwampashi imeweza kukagua jumla ya miradi sita ikiwemo ya elimu katika Kata ya Chitete,afya hospitali ya Itumba,umeme katika Kata ya Mlale mradi wa maji Ntembo na barabara Kata ya Ikinga.
Kwenye ujenzi wa shule ya msingi Ikumbilo kupitia fedha za BOOST imeagiza uongozi wa wilaya kujipanga upya kwani kasi si hairidhisha ikilinganishwa na maeneo mingine katika mkoa
Kwenye mradi wa maji Ntembo wajumbe walifurahishwa ubora wa mradi pamoja na maelezo ya mkandarasi wakiwataka viongozi wa wilaya kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa wakandarasi kama walivyofanya kwa huyo wa mradi wa maji.
Mradi mwengine uliowafurahisha wajumbe ni ule wa ujenzi wa barabara ya Landani-Kiwira kutoka kwenye machimbo ya makaa ya mawe Kabulo kuelekea kiwanda cha makaa ya mawe Kiwira km 5 .
Kilichowafurahisha wajumbe ni namna mkandarasi anavyofanya kazi kwa umakini huku akishirikisha jamii inayozunguka mradi kwa kutoa ajira za muda.
Kwenye hospitali ya Itumba ambayo ni ya wilaya mambo hayakwenda vema kwani Mwenyekiti wa CCM mkoa alitoa maagizo mazito kwa viongozi wa wilaya huku akikemea tabia ya uzembe kwa baadhi ya watumishi wanaofanya kazi kwa mazoea.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa