Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Anna Gidarya mapema leo Alhamisi Desemba,29,2022 alipoongoza Kamati ya Usalama kukagua Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya pamoja na Kituo cha Afya cha Ndola.
Akiwa Ndola kiongozi huyo hakuridhishwa na kasi,viwango vya ubora pamoja na nidhamu ya uzingatiaji wa maagizo ya viongozi wa ngazi mbalimbali za serikali kuanzia taifa,mkoa hadi wilaya.
Alisema kuwa pesa za mradi wowote wa serikali zinapotolewa katika halmashauri haziwi za idara husika pekee,bali ni kwa wote kutakiwa kujua kiasi cha pesa kilichotolewa,pokelewa,namna mradi utakavyotekelezwa,uwazi kwa wajumbe wa kamati za usimamizi pamoja na wananchi wote.
Mhe.Gidarya aliongeza kuwa idara inayohusika inapokuwa haiweki wazi taarifa kuhusu mradi na wengine kuamua kususia kwa kukosa taarifa kisha kukaa kimya wakisubiri mradi ukwame ni jambo lisilokubalika.
Alisema kuwa mradi unapoharibika inakuwa si aibu ya mtu mmjo au watu wachache bali taasisi nzima kisha huchafua taswira ya serikali mbele ya wananchi ambao wanakuwa na matumaini na matarajio makubwa juu ya mipango ya serikali katika kuwaletea maendeleo.
Mhe.Mohamed Mwala Diwani wa Kata ya Itumba palipo na hospitali ya wilaya akizungumza kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi alishukuru serikali kwa kuendelea kutao mamilioni ya fedha kwaajili ya miradi ya maendeleo huku akishauri ulinzi na ufuatiliaji wa fedha hizo pamoja na utunzaji wa vifaa vya ujenzi uongezwe mara dufu kwenye maeneo ya miradi.
Miradi ya maendeleo ya serikali kila inapotekelezwa hupitiwa na mamlaka mbalimbali zikiwemo Kamati za watalaam za halmashauri,Usalama za Wilaya,Wahe.madiwani,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Kamati za Bunge,wafadhili wa miradi husika,Wahe.Mawaziri pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya Taifa,mkoa na wilaya wakijiridhisha namna Ilani ya Uchaguzi inavyotekelezwa na kupunguza kero kwa wananchi.
Wilaya ya Ileje imeendelea kunufaika na mamilioni ya fedha zinazotolewa na serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo matokeo yake yanaonekana kwenye ujenzi wa vyumba vya kisasa vya madarasa,miundombinu ya barabara afya,mikopo kwa vjiana,wanawake,wenye ulemavu pamoja na mikopo ya bei nafuu ya pembejeo za kilimo.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa