Thursday 3rd, April 2025
@Daraja la Mto Songwe katika Kijiji cha Isongole hadi mpakani na Kijiji cha Izuba
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe jana Jumamosi tarehe 23,Januari,2021 aliwaongoza wananchi wake kupanda miti kando kando ya barabara ya Mpemba-Isongole inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na zaidi ya km 50.
Katika zoezi hilo zaidi ya miti 4000 ilipandwa na kutoka Daraja la Mto Songwe ambao ni mpaka kati ya Tanzania na Malawi hadi mpakani mwa Kijiji cha Isongole na Itumba.
Miche ya Miti hiyo imtolewa na Wakala wa Misitu Tanzania TFS,huku pia wananchi wakipata miche ya kupanda majumbani kwao.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa