Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na uvuvi Bw. Andrew Peter Mtui ametoa rai kwa kikundi cha maendeleo cha vijana ambao ni wanufaika wa mkopo wa asilimia kumi unaotolewa na Halmashauri , kuhakikisha wanarejesha Mkopo kwa wakati ili kutoa nafasi kwa Vikundi vingine kupata Mkopo kwa awamu nyingine.
Akizingumza wakati wa Hafla ya kukabidhi pikipiki 6 zilizogharimu Shilingi Milioni 15.5 kwa Kikundi cha Vijana wanaojishughulisha na huduma za usafirishaji ( bodaboda ) kutoka Kata ya Mbebe, Bw. Mtui amewasisitiza vijana hao kuzingatia sheria za usalama barabarani Pamoja na kuvitunza vyombo hivyo vya usafiri ili kuleta faida iliyokusudiwa.
Aidhaa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amewaasa vijana hao kuwa na nidhamu ya fedha Pamoja na kutunza familia zao kupitia kipato watakachokipata kupitia huduma za usafirishaji watakazokuwa wakizitoa katika jamii.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa