Mkuu wa wilaya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi, Amewahimiza wananchi wa Kata ya Bupigu wilayani hapa, Kuishi kwa kuzingatia misingi bora ya afya ili kuepuka magonjwa ya milipuko inayotokana na kutokuzingatia Kanuni za afya.
Mheshimiwa Mgomi, amewataka wananchi wa kata hiyo kuchukua tadhahari dhidi ya magonjwa ya mlipuko kwa kuzingatia usafi wa mazingira, usalama vyakula na matumizi ya vyoo bora, ili kuepuka magonjwa kuhara na kutapika yanayosababishwa na uchafu.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa Rai kwa Wakazi wa Kata hiyo, kuwa na utamaduni wa kutumia Choo Bora, Sambamba na matumizi ya maji safi salama ili kuepuka magonjwa kama kuhara na kutapika ambayo husababishwa na uchafu kwa kutokuzingatia kanuni za usafi .
Mheshimiwa Mgomi aliambatana na timu na wataalam wa Afya, Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Vijijini (RUWASA) pamoja na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ambapo kwa pamoja walitoa elimu kuhusu misingi bora ya Afya Pamoja na elimu ya usalama na uraia.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa