Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi Amewaongoza Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, Katibu Tarafa ya Bulambya Bi Irene Lyimo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje Bw. Peter Andrew Mtui pamoja na Wataalamu na Wakuu wa Idara mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, kutembelea na kukagua utekelezwaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo wilayani hapa.
Ziara hiyo imefanyika mapema leo February 11, 2025 ambapo Mkuu wa Wilaya amewahimiza wasimamizi wa Miradi hiyo kuendelea kuzingatia Ubora, Ufanisi pamoja na kuongeza kasi katika utekelezwaji wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi katika wilaya hii.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa siku ya leo ni pamoja na Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ubatizo Songa iliyopo Kata ya Bupigu, Mradi wa Ujenzi wa Vyumba viwili vya Madarasa na Vyoo Shule ya Msingi Mpakani iliyopo kata ya Isongole, Mradi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Ileje, Mradi wa Ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) Hospitali ya Wilaya iliyopo Kata ya Itumba pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Jengo Jipya la Utawala la Halmashauri ya wilaya ya ileje.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa