Serikali imeridhishwa na kasi na ubora wa majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Ileje na ikiahidi kumwaga milioni 500 zingine kwajili kuendeleza ujenzi huo.
Akizungumza kwenye eneo la mradi na baadaye ukumbini Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo aliwapongeza viongozi wa Wilaya hiyo kwa usimamizi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya baada ya serikali kutoa Bilioni Moja na Milioni 500.
“Katika Halmashauri ninayoweza kuwapa credit watumishi wa umma ninyi Ileje mmefanya maamuzi sahihi,kwakweli niwasifu hospitali yenu ni nzuri na itakapokamilika itakuwa kama Hospitali zingine za rufaa hapa nchini”.
Alisema kuwa kinachotakiwa ni kuongeza nidhamu kwenye matumizi ya fedha zikiwemo milioni 200 zilizobaki na milioni 500 zingine zitakazotolewa tena.
Aliwataka Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kujipanga kabla fedha hizo hazijatolewa ili zinapoletwa zianze kutumika mara moja.
Pia Mhe.Jafo aliwataka watumishi wa umma kijiamini wanapofanya kazi,wakiimarisha ushikiano ili miradi ya maendeleo iweze kusimamiwa ipasavyo.
Pamoja na mambo mengine Waziri huyo alizitaka Halmashauri kuhakikisha kuwa zinakusanya mapato ya ndani na kuziba mianya yote inayoweza kupoteza mapato hayo.
Kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kutakuwa ni ukombozi kwa wananchi ambao kwa muda wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya ikiwemo kwenda nchi jirani ya Malawi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa