Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Ndg.Omary Mgumba akiwa katika ziara yake ziara yake ya kwanza ya kutambua eneo la utawala tangu kuteuliwa kwake.
Alisema kuwa Mungu aliwapeleka Ileje kwa makusudi hivyo hawana budi kuchapa kazi wakigeuza changamoto hizo kuwa fursa badala ya kuwa na fikra za kuhamia maeneo mengine ambayo fursa nyingi zilishakabwa na wajanja.
Alisema kuwepo kwa mpaka na nchi ya Malawi kwa sehemu kubwa ya wilaya hiyo kunatoa fursa za uwekezaji badala ya kuendelea kulalamika kuwa mazingira ya Wilaya hiyo ni magumu.
Kauli hiyo ilikuja kufuatia taarifa ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt.Seif Shekillage anayehama kuwa watumishi wengi wa wilaya hiyo hususani walimu wamekuwa wakihama kwa idadi kubwa ikilinganishwa na Wilaya zingine katika mkoa huo.
Mgumba aliongeza kuwa kukamilika kwa barabara ya lami kati ya Mpemba na Isongole ni fursa kubwa kwa watumishi na wafanyabiashara wa wilaya hiyo,mkoa na taifa kwa ujumla katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Pamoja na mambo mengine kiongozi huyo amewataka watumishi wa umma kutokuwa chanzo cha migogoro ya kisiasa baina ya Wahe.Wabunge na wananchi wakisema hawaonekani majimboni wakati wanajua wazi kuwa wapo bungeni kuwawakilisha.
Amesema kuwa uelewa wa wataalam hao unatakiwa kuwa msaada wa kutoa uelewa wa mambo mbalimbali kwa wananchi badala ya kuwa wachochezi.
Ziara hiyo imemwezesha pia kukutana na watumishi wa umma,kutembelea Mradi ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari Kakoma pamoja na mpaka wa Tanzania na Malawi katika Kijiji cha Isongole ambako ujenzi wa daraja litakalounganisha Tanzania na Malawi unaendelea vema.
Tangu kuanzishwa kwa mkoa huo takribani miaka sita iliyopita Mhe.Mgumba anakuwa Mkuu wa Mkoa huo wa tatu akitanguluwa na Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela pamoja na Mhe.Mstaafu Chiku Galawa.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa