Tahadhari hiyo,imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Farida Mgomi alipokuwa akifunga kikao cha watalaam wa ngazi ya wilaya,kata na shule watakaotekeza mradi huo kwa mara ya kwanza baada ya wilaya kupokea Tzsh.1,574,100,000/=
Mgomi amewataka wahusika kushikamana akiongeza kuwa fedha hizo hazijalengwa kwa Idara ya Elimu Msingi tu bali ni kwa halmashauri nzima hivyo kufanikiwa sifa inakuwa ya wote hata kutofanikiwa inakuwa hivyo pia.
Ameongeza kuwa hatawavumilia wale wote watakaokwamisha miradi hii kwa namna yoyote ile wakiweka maslahi yao binafsi badala ya maslahi ya umma.
Serikali chini ya Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa fedha hizo ambazo zitazinufasha shule nane kwa kujenga vyumba vya madarasa,matundu ya vyoo pamoja na nyumba ya walimu.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa