Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje na pia Mkuu wa Idara ya Kilimo , Mifugo na Uvuvi katika Halmshauri ya Wilaya ya Ileje Bw. Peter Andrew Mtui amewaasa Wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayopambana Kuimarisha na Kuboresha Ustawi wa Watanzania kwa kuleta Maendeleo katika Nyanja zote ikiwemo sekta ya Afya.
Akizungumza katika Hafla ya kukabidhi msaada wa Betrii la kuongeza nguvu ya umeme jua (solar batteries) katika Zahanati ya Ighoje iliyopo Kijiji cha ilondo kata ya Malangali wilayani hapa, ambao umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ileje Mheshimiwa Mhandisi Godfrey Kasekenya, Mtui amesiwasisitiza Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kuhakikisha dhana nzima ya Ustawi kwa kila Mtanzania inakamilika.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amemshukuru Mbunge Jimbo la Ileje Mheshimiwa Mhandisi Gofrey Kasekenya kwa kukabidhi msaada huo wa Betrii ili kuimarisha huduma za Afya katika Zahanati hiyo, kwani kupitia betrii hiyo Zahanati itaendelea kupata huduma ya umeme katika nyakati zote hali itakayoboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi wa Kitongoji cha Ighoje.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa