Na;Daniel Mwambene,Bupigu-Ileje.
Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama(katikati) akimwonyesha Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mh. Joseph Mkude(kulia) madhara ya kukatwa kwa mti huo.
Serikali wilayani Ileje mkoani Songwe imewataka wananchi kushikamana katika kulinda miti ya asili ikiwa ni njia mojawapo ya kulinda rasilimali ya maji.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bupigu Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mhe,Joseph Mkude aliwataka wananchi hao kutoingiza itikadi za kisiasa katika kulinda mazingira.
Alitoa kauli hiyo,kufuatia kukatwa na kuangushwa kwa mmojwapo wa miti mikubwa katika kijiji hicho kwa malengo ya ujenzi wa shule na kuharibu ikolojia ya mahali pale alisema matokeo ya uharibifu huo yana madhara kwa watu wote bila kujali tofauti zao.
Mto huo uliokuwa karibu na Mto Songwe ulio mpaka kati ya Tanzania na Malawi ulipokatwa ulileta mvutano kati ya mamlaka zinazohusika na kulinda rasilimali za Taifa ikiwemo miti hiyo ya asili.
Wakati wa vikao kadhaa na wananchi walimweleza kiongozi huyo kuwa walikata mti huo kwaajili ya ujenzi wa shule kwa kuwa miti hiyo hawezi kuliwa kwa urahisi na mchwa ambao ni tatizo kubwa katika Tarafa ya Bulambya.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Ndugu Jackison Mwenga alimwomba kiongozi huyo kuendelea kutoa elimu ya mazingira kwa vile wamekuwa wakiishi kwa mazoea bila kujua kuwa baadhi ya shughuli hizo zinachangia kuharibu mazingira.
Uchunguzi umebaini kuwa kutokana na ukubwa wa mti huo zaidi ya mbao 300 zinatarajiwa kupatikana huku ukujaji wake ilikufikia kiwango hicho ni zaidi ya miaka 100.
Akijibu hoja hiyo na nyinginezo Mh. Mkude aliwataka wananchi hao kubadilika kwa kuanza kutumia mbao nyeupe ambazo zinatokana na miti ya kupandwa kwa kupaka dawa za kuzuia wadudu hao.
Kumekuwa na matukio kadhaa ya baadhi ya wananchi wilayani humu kukata miti kwaajili ya shughuli mbalimbali yakiwemo matumizi ya nyumbani,ujenzi na nishati.
Sehemu ya mti uliokatwa katika kijiji cha Bupigu wilayani Ileje na kuharibu ikolojia ya sehemu hiyo.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa