Zoezi hilo liliongozwa na Kaimu Afisa Elimu Msingi Wilayani Ileje Mkoani Songwe Mwl.Bashiri Msegeya ambaye ndiye msimamizi wa kitengo hicho .
Shule zilizonufaika na mgao huo ni pamoja na shule ya Msingi Ikumbilo Kata ya Chitete ambako mtoto Gift Sichinga mwenye matatizo ya ngozi alipokea mafuta maalum ya kupakaa,kofia na miwani maalum itakayomsaidia kukabiliana na jua.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo mtoto huyo aliishukuru serikali kwa msaada huo akisema utaongeza usalama wa ngozi yake inayodhurika juani.
Zoezi hilo liliendelea hadi Shule ya Msingi Mbebe ambapo pana Darasa la watoto 19 wenye mahitaji maalum ambapo wamepokea vifaa vya kuchezea pamoja na mabango mbalimbali ya kujifunzia.
Akizungumza shuleni hapo Afisa Elimu huyo alisema kuwa hivi karibuni Wilaya hiyo inatarajia kuanzisha kitengo maalum cha watoto wa mahitaji maalum katika shule hiyo na hivi karibuni mwalimu aliyesomea masuala hayo ataanza usimamizi wa kitengo hicho.
Hadi sasa Wilaya ya Ileje ina jumla ya shule nne zenye madarasa ya watoto wenye mahitaji maalum ambazo ni Ilulu,Mkumbukwa,Ikumbilo na Chitete uteuzi wa shule hizo ukizingatia wingi wa watoto wa aina hiyo kutokana na sense inayoyofanywa mara kwa mara.
Wilaya hiyo ikitekeleza hayo tayari serikali ilishaunda Wizara Maalum inayoshughulikia masuala hayo lengo likiwa ni kuhakikisha watu wa aina hiyo wanapata haki zao za msingi ikiwemo elimu.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa