Wakizungumza shuleni wanafunzi wa shule hiyo walibainisha namna wanavyofaidika na TEHAMA katika kujifunza,huku wakipongeza juhudi za wazazi,walimu na serikali kwa ujumla katika kufikia hatua hiyo
Wanafunzi hao wa Darasa la Saba walikutwa darasani kwao wakitumia vifaa vya TEHAMA Ikiwemo komputa mpakato pamoja na projekta kufanya maswali huku mwendeshaji mongozaji wa vifaa hivyo akiwa mwanafunzi
Akielezea mafanikio ya shule hiyo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo alisma kuwa lengo lao kuu ni kuhakikisha madarasa yote yote yanafikiwa na TEHAMA.
Kwa miaka kadhaa sasa Tanzania ikiwa sehemu ya Ulimwengu imendelea kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji katika kuiendeleza sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuwa sehemu ya Dunia ni Kijiji kimoja.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa