Pongezi hizo zinakuja ukiwa umepita karibu mwaka mmoja tangu wakazi hao walipofikisha kilio chao kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Omary Mgumba aliyekuwa kikazi wilayani humo wakitumia mtindo wa kukaa na kulala barabarani wakizuia msafara.
Timotheo Mwamahonje mwenyekiti wa Kijiji cha Itale akizungumza kwa niaba ya wakazi wa kata hiyo ameshukuru zao viongozi wa ngzi mbalimbali kuanzia Mhe.Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan,Wahe.wabunge,Mkuu wa Mkoa,Wilaya,pamoja na Baraza la Madiwani kwa kufanikisha ujenzi wa kituo cha afya kuanza baada ya kupokea milioni 500 za Kitanzania
Naye diwani wa kata hiyo,Mhe.Fahari Mwampashi ameishukuru serikali kwa mamilioni ya pesa kutua katani kwake
Akizungumza katika eneo la mradi,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Ubatizo Songa alipongeza umoja uliopo kwa Wahe.Madiwani,watalaam,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na wananchi wote akisema kuwa huwezesha michakato ya miradi ya maendeleo kukamilika.
Pamoja na mambo mengine aliipongeza serikali kwa kuwezesha mradi wa maji katika kijiji hicho akisema yamepunguza gharama za ujenzi pia.
Kuendelea kutolewa kwa mamilioni ya pesa kwenye maeneo mbalimbali ndani ya wilaya ya Ileje na Tanzania kwa ujumla ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama inavyojieleza kuhusu masuala ya afya kwenye katika kujenga hospitali,vituo vya afya,zahanati,ununuzi wa vifaa tiba pamoja na kuajiri watalaam.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa