Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Ajira,Mafunzo na Maendeleo ya Walimu(TSC) Bi.Christina Happy wakati akizungumza na Maafisa Utumishi,viongozi wa elimu wa Wilaya ya Ileje pamoja na walimu wa Kata ya Itumba ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya hiyo.
Alisema kuwa mawasiliano yakiwa mazuri yanarahisha upatikanaji wa taarifa za vitendo vya ukatili hata kwa watoto wa kiume wanaolawitiwa pasipo wao wenyewe kujieleza kwa vile tu imezoeleka katika jamii kuwa wanaonyanyashwa mara nyingi ni watoto wa kike.
Aliongeza kuwa wanafunzi wakijingewa urafiki wa kusikilizwa na walimu wao wataweza kutoa taarifa za aina hiyo ,hivyo kuwezesha sheria za nchi kuingilia kati na hatimaye kuongeza usalama wao.
Aidha kiongozi huyo alipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa jinsi wanavyotoa ushirikiano kwa Ofisi ya Tume ya Utumishi ya Walimu katika kuhakikisha kuwa huduma kwa walimu pamoja na maadili ya ualimu yanazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kwa pamoja walimu wanaokiuka maadili hayo.
Walimu kwa upande wao walimwomba kiongozi huyo kuhakikisha anafikisha kilio cha madai yao na haki mbalimbali kwa viongozi hali itakayoongeza utenaji kazi unaoleta matokeo chanya.
Asalile Kabuje mwalimu toka shule ya Msingi Rungwa amesema viongozi wa ngazi mbalimbali hawana budi kuwa chanzo cha kuwatia moyo wa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya elimu.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa