Zaidi yam ashine sita za kubangua karanaga katika kijiji cha Isongole Wilayani Ileje zimehamishwa kutoka eneo la soko na kupelekwa kwenye eneo lililotengwa kwaajili ya viwanda katika Kitongoji cha Chumbageni A.
Kuhamishwa kwa mashine hizo kunatokana na mpangilio sahihi wa makazi ambapo enelo walilohamishiwa wajasiliamali hao ndilo sahihi kwa shughuli za viwanda vikiwemo viwanda vidgovidogo kama hivyo.
Wakizungumza katika eneola tukio baadhi ya wajasiliamali hao wamesema kuwa wameridhishwa na kuhamia katika eneo hilo kwani mara kwa mara walikuwa wakiingia katika migogoro na majirani zao wa kibishara kwa tuhuma za kuchafua mazingira kutokana na kelele,vumbi pamoja na maganda ya karanga.
Isaya Ngabo mmoja wa wamiliki wa mashine hizo alisema kuwa amesema ana amini kuwa eneo hilo nisahihi kwao na hawatakuwa kero kwa watu kama lilivyokuwa lile la awali la soko.
Hata hivyo ameomba TANESCO kutupia macho katika eneo hilo ili ili kuwaondolea kero ya umeme ambayo kwa siku tatu walizofanya kazi hapo imekuwa inapunguza kasi ya uzalishaji kwa wanaamini kuwa umeme uliokuwa umepelekwa hapo awali ulilenga matumizi ya nyumbani na si viwanda.
Naye Pendo Kajange mmoja wa wateja wanaobangua karanga katika mashine hizo amesema kuwa kuyumbayumba kwa umeme kunakwamisha kasi na kupoteza muda mwingi katika mashine hizo na kukwamisha shughuli zingine.
Andinginie Kamwela mkazi wa kitongoji hicho ameelezwa kukerwa kwake na hali ya umeme kuyumbayumba na kuathiri matumizi yake ndani ya nyumba zao.
Eneo hilo kwaajili ya viwanda lilitengwa na halmashauri ya wilaya ukiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi inayoelekeza upangaji sahihi wa matumizi ya ardhi.
Katika ziara yake miaka kadha iliyopita Waziri Mkuu wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Mkoani Songwe aliagiza kila halmashauri kuwa na mpango mzuri wa ardhi ili kuepusha migogoro,hali ambayo Ileje imeendelea kutekeleza kwa kupima viwanja katika kijiji cha Isongole mpakani na Malawi pamoja na Ipapa.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa