Kampuni ya Kichina GEO Engeneering inayojenga barabara ya Mpemba hadi Isongole mkoani Songwe imetoa vifaa mbalimbali kwaajili ya shule za Msingi na Sekondari wilayani Ileje ukiwa ni uchangiaji wa huduma za kijamii.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na madawati na viti zaidi ya 200, mipira ya michezo pamoja na redio 80 kwaajili ya sekta hiyo muhimu hapa chini na Duniani kwa ujumla.
Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Generali Nicodemas Mwangela aliwataka wanafunzi kuthamini na kudumisha mahusiano na mataifa kama China yenye malengo mazuri kwa muda mrefu na Taifa letu.
Ndugu Joseph Mkude Mkuu wa Wilaya hiyo alishukuru kwa msaada huo akisema kuwa kuna shule zilikuwa katika mahitaji makubwa ya vifaa vya michezo ikiwemo shule ya Msingi Igumila iliyopo kata ya Ndola.
Hata hiyo DC huyo alitoa angalizo kuwa kamwe misaada hiyo isiwe chanzo cha kujibweteka bali mipango ya wananchi katika kujiletea maendeleo iendelee kutekelezwa kwa nguvu zote.
Mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo aliitaka jamii kuongeza nguvu katika uwekezaji kwenye elimu akisema kuwa hiyo ni njia pekee ya Tanzania kujipatia heshima mbele ya mataifa mengine.
Makabidhiano ya vifaa vyote yalifanyika katika Sekondari ya Kakomaliyopo kata ya Chitete palipo na kambi la ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu zaidi ya kilometa 50.
Vifaa hivyo vinatarajiwa kugawawiwa kwa shule mbalimbali za Sekondari na Msingi ambako maafisa Elimu Msingi na Sekondari waliahidi kusimamia utunzaji wake.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa