Akifungua kikao cha kwanza hivi leo Jumatano kwa watalaam toka Halmashauri hiyo watakaohusika na usimamizi wa Mradi huo unaojumuisha nchi za Tanzania na Malawi Mkurugenzi Mtendaji Haji Mnasi alizishukuru serikali zote mbili kwa jinsi zinavyohangaikia mradi huo ili kufikie malengo yake
Mnasi,alisema kuwa mradi huo utaimarisha mahusiano ya nchi hizo na kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi wa mpakani hali itakayoongeza pia mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Katibu Mtendaji Sekretariaeti ya Bonde la Mto Songwe Mhandisi Gabriel Kalinga alisema kuwa mradi utahusu ujenzi wa mabwawa matatu katika Kata za Bupigu,Malangali na mpakani mwa Wilaya za Ileje na Kyela.
Mhandisi Kalinga aliongeza kuwa lengo la mradi huo ni kukabiliana na kubadilika kwa mpaka kutokana na kuhama hama kwa mto Songwe kunakosababishwa na uharibifu wa mazingira na hivyo kuleta nadhara makubwa kijamii,kisiasa na kiutawala.
Hapo kesho Alhamisi kunatarajiwakufanyika kwa vikao vya Wakuu wa Idara na Vitengo huku Ijumaa ya Tarehe 29/5/2020 kukitarajiwa kikao cha Wahe.Madiwani
Mradi wa Bonde la Mto Songwe unausisha Wilaya tano kwa upande wa Tanzania ambazo ni Ileje,Kyela,Mbeya Vijijini,Mbozi na Momba huku Wilaya za Chitipa na Karonga zikiwa upande wa Malawi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa