Ileje-Songwe
Karibu vijana 50 wanatarajia kuanza rasmi mafunzo ya Ufundi Stadi katika Chuo cha VETA kilichopo Wilayani Ileje Mkoani Songwe hapo siku ya Jumatatu juma lijalo.
Akizungumza katika maeneo hayo Mkuu wa Chuo hicho Ndg.Joseph Mkiwa alisema kuwa kati ya vijana hao 38 watajiunga na kozi ya umeme wa majumbani huku vijana 12 wakijiunga na kozi ya ushonaji.
Alisema kuwa,jumla ya waliosajiliwa ni 50 huku walioripoti tayari kwa masomo hapo Jumatatu ni 12 wakifanya usafi wa mazingira na jumla ya walimu sita wa fani mbalimbali walisharipoti.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa,kozi za udreva na kompyuta zitakuwa zikifundishwa muda wowote kutegemeana na idadi ya wahitaji watakaojitokeza
Aidha alibainisha kuwa somo la kompyuta ni la lazima kwa kozi zote ili kwenda sanjari na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani.
Hata hivyo,Ndg.Mkiwa alionesha wasiwasi juu ya idadi ndogo ya wanachuo walioripoti mpaka sasa ikilinganishwa na idadi waliojisajiri ingawa viwango vya ada havizidi 210,000 kwa mwaka.
Chuo hiki ambacho ni cha serikali kinaifanya wilaya ya Ileje kuwa na vyuo viwili kingine kikiwa Chuo cha Ufundi Isongole kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini vikiongeza ajira kwa vijana.
Akizungumzia suala la uwepo wa fursa hizi Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg.Joseph Mkude aliwataka vijana kuzichangamkia ili kuepuka kukimbilia shughuli moja kwa kila kijana anayemaliza kidato cha nne kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo,huku fursa hizo zikichukuliwa na watu wa mbali.
Kauli hiyo imekuja kufuatia taarifa ya Mkuu wa Chuo hicho kuwa wengi walioripoti wanatoka nje ya wilaya ya hiyo ingawa walishasajiliwa.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa