Vigogo wa upinzani Ileje wahamia CCM
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapa nchini vigogo wanne wa vyama vya siasa vya upinzani wilayani Ileje vimepoteza majembe yake baada ya kuhamia CCM ili kuijenga Tanzania mpya kama walivyosema.
Waliokabibdhi kadi zao za vyama vya awali kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Songwe na kupewa kadi mpya za kijani ni pamoja na Ndg.Pitirosi Mshani aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Itumba ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Ileje.
Wngine ni Ndg.Francis Mbembela aliyegombea udiwani kata ya Isongole 2015 kupitia ACT Wazalendo akitokea CHADEMA ambako aliwahi kuwa kiongozi pia,Eliamu Kibona pia (CHADEMA) alikuwa ni mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Itumba pamoja na mama Dale Kaonga aliyekuwa tishio upande wa wanawake kisiasa akitokea CHADEMA.
Wakizungumza mara baada ya kupokelewa na Katibu wa Mkoa wageni hao waliahidi kukitumikia chamaa hiki na kuhakikisha kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi huu.
“Kazi zinazofanywa na Awamu hii haziwezi kupingwa kwa lolote kwani zinalenga kuwakomboa watanzania,yeyote anayepinga matokeo ya kazi hizi atakuwa anapingana na Mungu”Alisema Ndg.Eliamu Kibona.
Akizungumza na wajumbe wa kikao kwenye Ukumbi wa CCM wilayani humo(maarufu kama Kimwaga) Bi.Mecy Moleri aliwataka wanachama wa CCM kuungana na wanachama hao wapya katika kazi mbalimbali za chama ikiwemo mipango ya ushindi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.
Naye,Diwani wa Kata ya Itumba Mhe.Mohamed Mwala alifurahia kupokea wageni hao akisema hakika chama kimepata majembe ya kazi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa