Zoezi la upimaji limeanza leo Jumanne 01,Februari,2022 katika Kijiji cha Isongole kwenye Kitongoji cha Chumbageni ‘A’ukiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM inayolenga katika uboreshaji wa makazi kwa wananchi wake.
Eneo hilo lipo mpakani kabisa likipitiwa na barabara iendayo nchi jirani ya Malawi kwa upande wa Tanzania ikiwa imejengwa kwa kiwango cha lami
Akizungumza kwenye eneo la kazi,Afisa Ardhi na Maliasili wa Wilaya hiyo Ndg.Dismas Ndinda alisema kuwa zoezi hilo litakapokamilika jumla ya viwanja 1800 vitakuwa vimepimwa katika eneo hilo pamoja na kwenye Kitongoji cha Ipapa kijijini hapo.
Ndinda ameongeza kuwa kutokana na fedha hizo,kifaa cha kisasa cha upimaji ardhi chenye thamani ya Milioni 37 kimenunuliwa hivyo kasi ya upimaji inatajiwa kuongezeka kwakuwa awali idara hiyo ilikuwa ikitegemea vifaa hivyo toka wilaya za jirani.
Afisa huyo alisema kuwa wanatarajia kuanza kuviuza viwanja hivyo mnamo mwezi Machi,2022 kwa bei zitakazotolewa hapo baadaye.
Hadi sasa Wilaya hiyo ilishapima viwanja vya makazi na biashara katika vijiji vya Itumba(ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya) pomoja na Isongole (eneo maarufu la biashara)
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa