Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geofrey Mizengo Pinda wakati wa ziara yake ya siku moja Wilayani Ileje mkoani Songwe alipotembelea Gereza la Ileje na kuzungumza na waandishi wa habari.
“Ni kweli wamekuwepo mahabusu ambao kesi zao nyingi zimekosa ushahidi ambao serikali haiwezi kuendelea kusimama nao mahakamani,watu kama hao hatuna sababu ya kuendelea nao” Alifafanua Mhe.Pinda.
Aliongeza kuwa ni muhimu Ofisi ya DPP kupitia mkakati wake kujaribu kupunguza kesi ili kuhakikisha kuwa mahabusu zetu zinapumua kwa kuondoa mlundikano.
Alisema kuwa kuna baadhi ya mahabusu na wafungwa wa nchi za nje wamekuwa wakituingizia hasara kwa makosa ambayo wangerudishwa tu makwao badala ya kuendelea kuwashikilia kihasara.
Akiwa gerezani hapo aliweza kuzungumza na wafungwa pamoja na mahabusu kwa kupokea kero na malalamiko yao akiahidi kuyafanyia kazi kupitia Ofisi ya DPP.
Katika ziara hiyo alifuatana pia na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe Mhe.Neema Mwandabila ambaye siku kadhaa zilizopita aliweza kutoa magodoro na mablanketi kwaajili ya wafungwa na mahabusu wa Gereza hilo la Ileje.
Mwanzoni mwa uongozi wake,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan aliziagiza mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za kuwaachia mahabusu wenye kesi zisizo na ushahidi,kisha tukashuhudia kuachiwa kwa Mashehe wa Uamusho.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa