Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi ameitaka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika Wilaya ya Ileje kuhakikisha wanamaliza mradi wa maji wa Itumba – Isongole kwa wakati ili wananchi wapate huduma bora ya maji.
Mheshimiwa Mgomi ametembelea na kukagua mradi huo wa maji katika wilaya hii, ambapo amewapongeza Ruwasa kwa jitihada walizozifanya katika Mradi huo ambao mpaka sasa umefikia asilimia 85% ili kukamilika na kuanza kutoa huduma.
Mradi wa maji wa Itumba – Isongole unatarajia kutoa huduma ya maji kwa wakazi wapatao 20,888 wa mji wa Itumba na Isongole ambapo jumla ya lita 3,201,000 zitazalishwa kwa siku ili kukidhi huduma ya maji kwa wakazi wa kata hizo katika wilaya ya Ileje.
Aidha mradi huo utaongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 63.9% ya sasa mpaka asilimia 100%.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa