Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi, ametoa rai kwa vikundi vya maendeleo vilivyopata mkopo wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kuhakikisha wanarejesha kwa wakati ili kutoa nafasi kwa vikundi vingine na kunufaika na huduma ya mkopo huo kwa awamu nyingine.
Akizungumza mapema leo wakati wa Hafla ya Kukabidhi Pikipiki 21 pamoja Pikipiki za Magurumu Matatu 2 vyenye thamani ya shilingi milioni 89,785,000/= kwa vikundi vitano vya ujasiriamali vinavojihusisha na huduma za usafirishaji katika wilaya ya Ileje, Dc Mgomi amewapongeza Wajasiriamali wa Wilaya hii kwa kujitokeza kusajiliwa ili wapate Vitambulisho vya Wafanyabiashara kwani vitawasaidia kutambulika na kupata Mikopo kwa Tasisi husika pamoja na huduma ya kufanya miamala mbalimbali Kidigitali.
Aidha amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yetu, Bi. Nuru Waziri Kindamba kwa kusimamia vyema mchakato mzima wa utoaji wa Mikopo ya Asilimia kumi ya mapato ya ndani na kuhakikisha inawafikia na kuwanufaisha walengwa husika .
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameviasa vikundi vilivyopewa pikipiki kuzingatia sheria za usalama bararabarani, kuwa na Nidhamu ya Fedha, pamoja na Kutunza Familia zao kupitia kipato watakachokipata kupitia huduma za usafirishaji watakazokuwa wakizitoa katika jamii.
Vikundi vilivyokabidhiwa pikipiki siku ya leo ni pamoja na Kikundi cha Never Give Up (Guta 2) Kikundi cha Kazi Iendelee ( pikipiki 3) Kikundi cha Chitulano ( pikipiki 3) Kikundi cha Jitegemee ( Pikipiki 5) pamoja na Kikundi cha Chapakazi (Pikipiki 10) zote zikiwa na thamani ya shilingi milioni 89,785,000/=.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa