Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Farida Mgomi katika viunga vya Halmashauri ya Wilaya hiyo mara baada ya kukabidhi pikipiki sita kwa baadhi ya maafisa hao.
Alisema kuwa vyombo hivyo vya usafiri vinatarajiwa kuwa chachu ya kuongeza utendaji kazi wa kila siku ikiwemo kufuatilia vikao,mikutano na shughuli za maendeleo katika vijiji vyao ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe.Ubatizo Songa Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo akizungumza katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji alipongeza juhudi hizo za serikali kwa kuwakumbuka watendaji hao walio karibu na wananchi.
Alisema kuwa pikipiki hizo zitaongeza kasi ya ukusanyaji mapato hususani kwenye kata za pembezoni zilizo mbali na Makao Makuu ya Wilaya ambako wamezielekeza yaani kata za Ikinga,Ngulugulu,Sange,Lubanda,Luswisi na Ngulilo.
Ndg.Rodrick Sengela Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo alishukuru serikali kwa mgao huo huku akiahidi kuwa wataendelea kuunga juhudi hizo za Mhe.Rais kwa kununua pikipiki hata kwa awamu kwaajili ya kata zilizobaki.
Ikumbukwe kuwa wilaya hiyo yenye tarafa mbili za Bundali na Bulambya ina jumla ya kata 18 hivyo kupatikana kwa pikipiki hizo sita kunaacha pengo la pikipiki 12.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa