Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mheshimiwa Farida Mgomi, amewapongeza Maafisa Watendaji wa Kata na Maafisa Lishe kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuboresha sekta ya lishe wilayan hapa. Pongezi hizo zilitolewa leo tarehe 27 Mei 2025, wakati wa kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya. Mheshimiwa Mgomi alisema kuwa juhudi hizo zimeanza kuonyesha mafanikio katika kupunguza viwango vya udumavu kwa watoto. Alisisitiza kuwa mafanikio hayo yanatokana na juhudi za pamoja kati ya serikali na jamii.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Mgomi amewataka watendaji wa Kata na Maafisa Lishe kuendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mikakati ya lishe. Alieleza kuwa lishe bora ni msingi muhimu wa afya ya watoto na maendeleo ya Taifa kwa ujumla. Alihimiza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii, kwa moyo wa kujitolea na Kujituma. Pia alisisitiza kuwa kila kiongozi anapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora.
Aidha Mkuu wa Wilaya ameaiahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha mipango ya lishe inatekelezwa kwa ufanisi. Alisema kuwa ofisi yake iko tayari kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuongeza uelewa wa jamii kuhusu lishe bora na kuboresha mazingira ya utekelezaji wa shughuli za lishe. Alihitimisha kwa kuwataka watendaji waendelee kuwa mabalozi wa lishe bora kwa wananchi wa Ileje, kwa kuhakikisha kila kaya inakuwa na uelewa na mbinu za kuandaa chakula chenye virutubisho vya kutosha.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa