Walimu hao wawili(ambao walikuwa marafiki enzi za uhai wao) Tumain Mwakyusa pamoja na Sunday Mwanjalila walipoteza uhai baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Kijiji cha Izuba wilayani humo na kupoteza uhai papo hapo.
Akihubiri katika ibada hiyo Askofu Akimu Mwinyilu wa Kanisa la EAGT wilaya ya Ileje aliwakumbusha watu wote kukumbuka kuwa sote tukiwa na mipango mingi ya kimaisha tunaweza kupoteza uhai muda wowote kama ilivyotokea kwa vijana hao.
Askofu Mwanyilu aliongeza kuwa ndoto zao zimekatishwa kwa muda mfupi hali inayoweza kumkuta mwanadamu yeyote.
Geofrey Nnauye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri hiyo alisema kuwa vifo hivyo vimetokea wakati wilaya ikiwa kwenye mchakamachaka wa kujikwamua kitaaluma vimeaccha pengo si kwa familia zao tu bali hata kwa taifa zima kutokana na utendaji wao.
Michael Ligola aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa akiwa Katibu Msaidizi upande wa elimu alipongeza umoja ulioneshwa na watu wote tangu mwanzo hadi ibada hiyo ilipokuwa ikifanyika.
Alisema kuwa watoto wote watano walioachwa na wazazi hao wawili wa kiume toka hizo familia mbili wanahitaji kuangaliwa kwa macho ya karibu na watu wengi ukiwemo mkoa ili kufikia ndoto zao.
Mhe.Ubatizo Songa Mwenyekiti wa Halmashauri aliitaka jamii nzima kudumisha yale mazuri waliyokuwa wakiyasimamia kila siku wapendwa hao
Wazazi wa marehemu kwa ujumla wao walishukuru viongozi wa wilaya,mkoa na wananchi kwa ujumla kwa namana wavyolibeba tatizo hilo tangu mwanzo.
Mauti iliwafika walimu hao Jumapili, 29 ,januari,2023 baada ya pikipiki kupata dosari katika kijiji cha Izuba Kata ya Isongole wakitokea Mbozi mwishoni mwa juma ambako iliielezwa kuwa ndiko familia zao ziliko.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa