Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bi. Nuru Waziri Kindamba ametoa tamko la kupiga marufuku shughuli za uchimbaji na ubebaji wa mchanga katika maeneo yote ya mito ili kuendelea kulinda maeneo hayo dhidi ya mmomonyoko wa udongo unaoweza kusababisha uharibifu wa mazingira pamoja na kubadili uelekeo wa mito ambayo inaweza kusababisha majanga katika makazi ya wananchi.
DED Kindamba ametoa tamko hilo kufuatia kuwepo kwa tabia ya wananchi kuchimba na kubeba mchanga katika mito ikiwemo mto unaokatisha maeneo ya National Housing katika Kata ya Itumba.
Utekelezaji wa agizo hilo unaanza mara moja.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa