Akizungumzia mafanikio yake kwa kipindi hicho aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg .Joseph Mkude amewashukuru viongozi wa kitaifa,mkoa,wilaya pamoja na wananchi kwa ujumla kwa jinsi walivyoshiriki katika kuijenga wilaya na kufanikiwa kuifikisha hapa ilipo.
Alibainisha baadhi ya miradi ambayo imefanyika katika kipindi chake kuwa ni ujenzi wa barabara ya Mpemba hadi Isongole kwa kiwango cha lami Zaidi ya km 50.
Mingine ni ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,vituo vya Afya vya Lubanda na Ibaba pamoja na utekelezaji wa Ilani juu ya ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji ambapo Zaidi ya zahanati 40 zimejengwa.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo,Mhe.Anna Gidarya amesema kuwa ana matarajio makubwa wa kupata ushirikiano kutoka kwa viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo katika kuwatumikia wananchi ili waweze kufikia malengo ya kitaifa katika ujenzi wa taifa.
Amesema kuwa ili kufikia malengo hayo lazima kutanguliza upendo na kuheshimiana kwa kuzingatia maelekezo ya mamlaka zinazotuongoza.
Makabidhiano hayo ni hatua ya mwisho kwa DC Joseph Mkude aliyehamia Wilaya ya Kishapu na nafasi yake ikichukuliwa na DC Anna Gidarya aliyeteuliwa hivi karibuni.
Mhe,Gidarya anakuwa Mkuu wa Wilaya wa nane tangu kuanzishwa kwa wilaya huku akiwa DC wa tatu wa mwanamke akipata nafasi ya kuwa moja wa wawakilishi wa wanawake katika kuongeza usawa katika uongozi na kupunguza fikra za mfumo dume.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa