Wakati Dunia nzima ipo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 wakazi wa Mkoa wa Songwe wametakiwa kuwalinda wanafunzi wa kike ili kuwaepusha dhidi ya mimba.
Wito huo ulitolewa na Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Songwe Mwl.Juma Kaponda anayesimamia Masuala ya Elimu alipokuwa akizungumza na umma kupitia Redio ya Kijamii ya Ileje Fm 105.3
Kaponda aliwataka Wanasongwe kuchukua hatua za ulinzi kwa wanafunzi wa kike ambao kwa sasa wapo majumbani ambako sheria za shule haziwabani .
Alisema kuwa mkoa wa Songwe unalo tatizo la mimba kwa wanafunzi hivyo ni hatari zaidi kipindi hiki kuingia katika tatizo hilo iwapo wadau hawatashikamana.
“Ndugu wananchi ikumbukwe kuwa huko uraiani kuna vijan wa Vyuo Vikuu,sekondari na vyuo vya Kati hali inayoweza kupelekea mahusiano mabovu yenye kusababisha mimba kutokea,kwani baada ya corona maishaya uanafunzi yataendelea kama kawaida” aliongeza kiongozi huyo.
Pamaja na mambo mengine Kaponda alizungumzia mikakati ya mkoa huo katika kuwasaidia wanafunzi kupata elimu kwa njia ya masafa ikiwemo njia ya mtandao kwa wanafanzi wa Kidato cha Sita.
Aidha,kupitia simu za wasikilizaji aliweza kupokea maswali,ushauri na pongeza kwa kutumia njia ya redio kuongea na wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani.
karibu miezi miwili imepita tangu kufungwa kwa shule na vyuo hapa nchini ukiwa ni muda mrefu ukilinganishwa na likizo zingine kukiwa na sintofahamu juu ya hatima ya gonjwa hili hatari..
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa