Katibu Tawala wa Wilaya ya Ileje, Abdallah Mayomba, amewapongeza wauguzi kwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii katika kuwahudumia wagonjwa. Amesema juhudi zao zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaohitaji huduma za afya, na kwamba wauguzi ni watu muhimu wanaotoa faraja wakati wa changamoto za kiafya.
Katika pongezi zake, Mayomba aliwatambua wauguzi kama nguzo ya faraja na matumaini kwa jamii, hasa katika mazingira ya hospitali na vituo vya afya. Alieleza kuwa moyo wao wa kujitolea unaleta tofauti kubwa katika maisha ya wagonjwa wanaowahudumia kila siku.
Pia alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya nchini, hali inayosaidia kurahisisha kazi ya wauguzi na kuboresha huduma kwa wananchi. Kauli hiyo aliitoa katika hafla ya usiku wa wauguzi iliyofanyika kwenye ukumbi wa RM, Itumba, wilayani Ileje.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa