Ileje yapokea vifaa vya kupunguza ya UKIMWI
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe imepokea vifaa mbalimbali vitakavyotumiwa na vijana wa umri katika ya miaka 15-19 kwenye Programu ya ”Ongea Redio’’.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na radio,simu pamoja flashi kwaajili ya vijana hao kusikiliza na kujadili vipindi vitakavyokuwa vikirushwa na baadhi ya vituo vya radio za kijamii katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Mbeya,Iringa,Njombe na Songwe.
Vipindi vilivyoandaliwa kwa njia ya michezo ya redio vinalenga kuokoa rika hilo dhidi ya maambukizi ya VVU na UKIMWI,jinsi ya kujikinga na mimba za utotoni pamoja afya ya uzazi vinatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika mpango wa taifa wa kufika asilimia sifuri ya maambukizi ya UKIMWI.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Ndugu Haji Mnasi huyo alishukuru akiahidi pia kusimamia matumizi sahihi ya vifaa hivyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Wilaya ya Ileje ni miongoni mwa wilaya mbili za mwanzo mkoani Songwe ikiwemo Mbozi kwa kuingizwa katika mpango huo ikiwa ni halmashauri pekee mkoani humo inayomiliki radio ya kijamii iitwayo Ileje FM 105.3 ambayo itatumika kutoa elimu kwa jamii kupitia mpango huo wa Ongea Redio.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa