Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Mhe.Farida Mgomi alipokuwa akizindua mradi huo katika Kijiji cha Ikumbilo Kata ya Chitete panapojengwa mkondo mpya wa shule ya Msingi Ikumbilo na inayotarajiwa kuwa shule kamili kutokana na mahitaji pamoja na kiasi hicho kikubwa cha fedha kilichotolewa naserikali.
Mgomi amewataka wasimamizi wa mradi ikiwemo Kamati ya BOOST ya wilaya kuwa na uwazi kwenye miradi hiyo ambapo serikali imetoa jumla ya Tzsh.1,574,1000,000/= kwa wilaya nzima huku mgawanyo wake ukizifikia shule nane ambazo ni Chitete,Ikumbilo,Ilulu,Ibezya,Ibaba,Sange,Mtula na Chembe huku shule mbili za kata hiyo zikipata kila moja Tzsh.347,500,000/=.
Kwa upande wao wananchi wamewataka kuwa walinzi wa kwanza wa mradi huo wakiwa wakihakikisha hujuma yoyote ya mradi haifanyiki katika maeneo yao,akiwahimiza kuripoti kwa vyombo husika juu ya matukio yoyote yanayoonesha kukwamisha mradi.
Aliongeza kuwa malengo ya serikali hayawezi kukamilika iwapo wananchi hawatatoa ushirikiano kwenye maeneo ya miradi kwa vile wao huona kila kiyu kinachofanyika kila siku na wakijua dhahili kuwa mradi ukiharibika wanaoumia ni wao.
Herman Njeje Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amewapongeza wakazi wa kijiji hicho kwa moyo wa uzalendo waliounesha ikiwemo kutoa eneo la shule pamoja na kujitokeza kufanya kazi siku hiyo ya uzinduzi wa mradi.
Aliongeza kuwa,nguvu ya wananchi inatakiwa ithaminiwe na kuthaminishwa ili fedha zinazookolewa zitumike kuongeza miundombinu mingine kwenye shule hizo.
Mhe.Osiwelo Chomo Diwani wa kata hiyo amewasihi wakazi wa kata hiyo kuendelea kutoa ushirikiano pindi wanapohitajika kutoa nguvu zao kwenye miradi hiyo pamoja na miradi mingine ya maendeleo huku akimwomba mwandisi wa ujenzi kuwa karibu na miradi ili kuepusha dosara zinazoweza kuzalisha marekebisho ambayo huongeza gharama za mradi.
Atanasi Ndimbwa mkazi wa eneo hilo ameishukuru serikali kwa kutoa kiasi hicho cha fedha huku akiahidi kuwa mlinzi wa mradi ili watoto wao waweze kufaidi matunda ya mradi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa