Ileje yatoa Elimu kwa Mpiga kura kwa njia ya redio.
Wakazi wa Ileje na maeneo jirani yanayofikiwa na masafa ya Redio ya Kijamii 105.3 Ileje FM wameweza kupata elimu ya mpiga kura kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019
Akizungumza na wananchi kupitia kituo hicho Msimamiziwa Uchaguzi Ndg.Godwini Mukaruka aliyefuatana na Afisa Uchaguzi wa Wilaya hiyo Bi.Lucy Mwani waliwaeleza wananchi juu ya sifa wanazotakiwa kuwa nazo wagombea wa nafasi za uongozi zitakazogombewa pamoja na sifa za mtu kujiandisha kuwa mpiga kura.
Mukaruka alisema kuwa watu wenye sifa hawana budi kujiandikisha ili kushiki kupiga kura ikiwa ni moja ya haki za raia wa Tanzania,akiwaasa wananchi kushiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu.
Baadhi ya wananchi walioweza kupiga simu za moja kwa moja kwa Msimamizi huyo waliomba mambo kadhaa yaweze kufanyiwa kazi ukiwemo muda sahihi wa ufunguaji wa vituo vya kupigia kura.
Msimamizi huyo anafanya zoezi hili zikiwa ni siku chache zimepita tangu akutane na wadu mbalimbali wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa dini na vyombo vya Ulinzi na Usalama vya wilayani humo.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hufanyika kila baada ya miaka mitano ukisimamiwa na TAMISEMI ambapo kwa mwaka huu unatarajiwa kufanyika tarehe 24 ,Novemba.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa